Monday, February 9, 2015

MFUMUKO WA BEI WAZIDI KUPOROMOKA

Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS imesema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Januari 2015 umeshuka na kufikia asilimia 4.0 kutoka asilimia 4.8 ya mwezi wa Desemba mwaka jana kutokana na kupungua kwa bei ya bidhaa na huduma ambazo ni pamoja na Mahindi, Unga wa Mahindi, Samaki na Mihogo pamoja na kushuka kwa bei ya nishati ya mafuta ikiwa ni pamoja na Mafuta ya taa.

0 comments:

Post a Comment